Taarifa Kutoka kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ikulu, ni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo February 14, 2018 amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Pamoja na uteuzi huo, Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.
Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwaambaye amestaafu.
Aidha, Rais Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali kama ifuatavyo
- Brig Jen. J.G. Kingu
- Brig Jen. M.S. Busungu
- Brig Jen. R.R. Mrangira
- Brig Jen. B.K. Masanja
- Brig Jen. G.T. Msongole
- Brig Jen. A.F. Kapinga
- Brig Jen. K.P. Njelekela
- Brig Jen. A.S. Bahati
- Brig Jen. M.E. Mkingule
- Brig Jen. S.S. Makona
Nb:Mabrigedia Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye. Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed ataapishwa kesho February 15, 2018 saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment