Ujumbe wa Korea
Kaskazini unaoongozwa na jenerali wa jeshi mwenye utata umevuka na
kuingia Korea Kusini kwa sherehe za kufungwa mashindano ya olimpiki ya
msimu wa baridi huko Pyeongchang.
Jenerali Kim Yong-chol
analaumiwa kwa kuzamisha meli ya vita ya Korea Kusini mwaka 2010 ambapo
wanajeshi 46 waliuawa. Korea Kaskazini inakana kuhusika.
Familia za waathiriwa na wabunge kadhaa wa Korea Kusini walifanya maandamano wakijaribu kuzuia ziara hiyo kwenye mpaka.
Ziara hiyo inafanyika wakati kuna kuboreka kwa uhusiano kati ya Korea hizo mbili.Wakati
wa mashindano ya olimpiki Korea Kaskazini na Kusini walitembea pamoja
chini ya bendera moja wakati wa sherehe za ufunguzi na baadaye wakawa na
kikosi cha pamoja na wanawake wa timu ya magongo.
Hata
hivyo wataalamu wanaonya kuwa yanayofanaika sasa hayamalizi kikomo
misukosuko ya kieneo hasa kufuatia majaribio ya nyuklia na ya makombora
yanayofanywa na Korea Kaskazini.
Ujumbe wa Marekani kwenye mashindano hayo
unaojumuisha binti wa rais Donald Trump Ivanka, umekana kukutana na
maafisa wa Korea Kaskazini.Siku ya Ijumaa Marekani ilitangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya korea Kaskazini.
Rasi ya Korea imegawanyika tangu vita vya miaka 1950 na pande zote mbili hazijawahi kuwa na makubaliano ya mkataba wowote.
No comments:
Post a Comment