masharti ya Korea Kusini kabla ya kukubali mualiko wa Kim Jong-un wa Korea Kaskazini - TANZA MEDIA ONLINE

Sunday, 11 February 2018

masharti ya Korea Kusini kabla ya kukubali mualiko wa Kim Jong-un wa Korea Kaskazini


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alimwalika mwenzake wa kusini kwa mkutano
Image captionKiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Waziri mkuu wa Korea kusini Lee Nak-yeon amebaini wazi kwamba kuna masharti ambayo lazima yabainishwe kabla ya kukubali mwaliko wa uongozi wa nchi hiyo kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong-un.
Jana katika hatua kubwa ya kidiplomasia kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alimwalika mwenzake wa kusini kwa mkutano lakini Rais Moon Jae-in bado hajatoa jibu la kuitikia wito huo au la.
Ujumbe huo umetolewa na dada yake kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong un ambaye aliandamana na maafisa wa ngazi za juu zaidi wa Korea Kaskazini kuwahi kuzuru Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya Korea miaka 60 iliyopita.
Hata hivyo hatua hiyo haijafurahiwa na Marekani ambayo ingali inataka kwanza Korea kaskazini ishinikizwe kuachana na miradi yake ya nyuklia.

No comments:

Post a Comment