Mama Mobeto.
KUFUATIA skendo nzito inayofukuta ya
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kutoka
kimapenzi na warembo, Wema Isaac Sepetu na Tunda Sebastian, mama mzazi
wa mwanamitindo Hamisa Mobeto, Shufaa Lutigunga ‘amemtapika’ jamaa huyo
kuwa vitu vyote vinavyoendelea kwenye mitandao ya kijamii havihusiani na
mwanaye.
Akizungumza na gazeti moja, mama Mobeto
alisema kuwa, kwa sasa, kwa upande wao, yeye na mwanaye Mobeto hawataki
malumbano na kuwekana kwenye mitandao wa kijamii ndiyo maana hawataki
kusikia habari zinazomhusu Diamond.
Alisema kuwa, muda huo wa malumbano
hawana kwa sababu mwanaye anaendelea na maisha yake mengine kabisa ya
kutafuta maendeleo na jinsi gani ya kuwalea watoto wake na si kumtegemea
mwanaume huyo.
Mobeto.
“Jamani sisi mambo hayo ya kwenye
mitandao muda huo hatuna tena. Hata mtoto wangu (Mobeto) ameshayasahau
mambo hayo na badala yake yupo bize na mambo yake mengine kabisa,”
alisema mama Mobeto.
Mama Mobeto aliendelea kueleza kuwa,
mtoto wake yuko kwenye mchakato mkubwa wa kufungua biashara yake ya
lipstiki hivyo muda wa kufuatilia chochote kinachoendelea kwenye
mitandao ya kijamii hana.
“Michakato yetu sisi zaidi ni kutafuta
pesa na si vingine. Muda wa kuchokonoana kwenye mitandao hatuna kwa
sababu tukifanya hivyo hatuwezi kupiga hatua hata siku moja, lakini kama
kuna watu wanaweza kufanya hivyo, wafanye kwani sisi tulishajivua siku
nyingi sana na wala hatutaki kumsikia huyo Diamond na mambo yake,”
alisema mama Mobeto.
chanzo: Risasi Jumamosi


No comments:
Post a Comment