MAHAKAMA YAWAACHIA MAJERUHI WA MAANDAMANO YA CHADEMA - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday, 28 February 2018

MAHAKAMA YAWAACHIA MAJERUHI WA MAANDAMANO YA CHADEMA

Image result for aida chadema


Majeruhi watatu waliopigwa risasi na polisi, na kushikiliwa kwa siku 13 bila kupewa haki yao ya matibabu, hatimaye wameachiwa kwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya jopo la wanasheria waliokua wakiwatetea, likiongozwa na Wakili Msomi Alex Massaba kuamua kuwashtaki IGP na Mwanasheria Mkuu kwa kosa la kuendelea kuwashikilia watu hao kinyume na Sheria.

Majeruhi hao Aida Olomi, Isaack lomanus, na Erick John wameachiwa huru leo baada ya wakili Massaba kufungua shauri Mahakama kuu hapo jana, akitaka IGP Sirro na Mwanasheria Mkuu, Dr.Kilangi waitwe mahakamani kujieleza kwanini wanaendelea kuwashikilia wateja wake kinyume na sheria na bila kuwapa haki yao ya matibabu.

Jaji Isaya Arufani alipokea shauri hilo na kutoa hati ya kuwaita mahakamani (summons) IGP na AG, kueleza ni kwanimi polisi inawashikilia mahabusu hao siku 13 bila kuwapeleka mahakamani..

Pia hii leo imebainika kuwa majeruhi wote watatu hawakupewa haki yao ya matibabu kama ambavyo Jeshi la Polisi lilieleza. Mwishoni mwa wiki iliyopita Mkuu wa Polisi Kinondoni ACP Muliro Jumanne alidai kuwa watuhumiwa hao walipatiwa matibabu jambalo si kweli. Leo baada ya kuachiwa wamelazimika kukimbizwa hospitali kupata matibabu.

No comments:

Post a Comment