Raia huyo wa Ufaransa alitoa mifano nchini ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Uhispania.PSG
iko pointi 11 juu katika ligi ya kwanza , Bayern Munich iko pointi 16
juu katika ligi ya Bundesliga na Manchester City ipo pointi 15 juu ya
jedwali la ligi ya Uingereza.
Wenger amesema kuwa ni wazi kwamba hakuna tena utabiri .
Aliongezea: Unapozitazama ligi tano barani Ulaya mnamo mwezi Disemba , unaweza kujua ni timu gani zitakazoshinda ligi zao.
Hiyo inamaanisha kwamba kunakitu hakiko sawa katika mchezo huu. Utajiri mkubwa wa baadhi ya timu unaharibu ushindani uliokuwepo.
Nchini
Uhispania, Barcelona ina pointi 11 juu ya jedwali la ligi dhidi ya
Athletico Madrid huku mabingwa watetezi Real Madrid wakikumbwa na msimu
mgumu, wako pointi 19 nyuma ya Barca katika nafasi ya nne.Ligi
nyengine ambayo inatamatisha ligi tano bora za Ulaya ni Italy ambapo
Napoli wapo pointi moja mbele ya Juventus ambao wameshinda taji hilo
kwa misimu sita mfululizo.
Wenger alikuwa akizungumza siku mbili
baada ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho nchini Uingereza
lililovunja rekodi kwa matumizi.Klabu za Uingereza zilitumia
£150m siku ya Jumatano ,katika siku ya mwisho ya uhamisho na hivyobasi
kujumlisha matumizi hayo kwa mwezi kufika £430m.
Kufikia mwisho wa dirisha la uhamisho mnamo mwezi Septemba , Wenger
alisema kuwa sheria ya Uefa ya Fair Play ilioanzishwa ili kukabiliana na
ubabe wa kifedha inafaa kufutwa kwa kuwa klabu haziiheshimu.
Mabingwa
wa Ufaransa PSG waliweza kulipa mara mbili ya ada ya uhamisho uliovunja
rekodi wakati walipomnunua Neymar kutoka Barcelona mwisho wa msimu
uliopita mbali na kumsajili Kylian Mbappe kwa mkopo ambao utamwezesha
kujiunga na klabu hiyo kwa dau la £165.7m mwisho wa msimu huu.
Manchester
City walishutumiwa kwa kutumia vibaya utajiri wao na rais wa ligi ya
Uhispania Javier Tebas ambaye pia alisema kwamba PSG ilikuwa ikiucheka
mfumo uliowekwa kutokana na ununuzi wao wa mwisho wa msimu.Mwezi
Januari matumizi ya klabu za Uingereza yalipiku yale ya wenzao wa Ulaya
licha ya Barcelona kulipa dau la juu wakati walipomnunua Phillipe
Coutinho kutoka Liverpool kwa thamani ya £142m.
Ligi ya Bundesliga imekuwa ikitawaliwa na Bayern
katika miaka ya hivi karibuni wakiwa wameshinda mataji 12 kati ya 18
ikiwemo mataji matano yaliopita mfululizo.Ni mara moja katika
misimu 13 iliopita ambapo taji la Uhispania limeshindwa na klabu
nyengine isipokuwa Real Madrid na Barcelona , ambapo Atletico Madrid
ilishinda 2014 .
Barca imelishinda taji hilo mara nane katika kipindi hicho huku Madrid ikilishinda mara nne.Nchini
Italy , Juventus imeshinda taji la Serie A kwa kipindi cha misimu sita
iliopita mfululizo huku Inter Milan ikishinda mataji matano kati ya
2006-2010.Nchini Ufaransa kulikuwa na washindi wa mataji sita
tofauti kati ya 2007-08 na 2012-13 lakini PSG imeshinda ligi hiyo katika
misimu minne kati ya tano iliopita.Kati ya 2002 na 2008 , Lyon ilishinda mataji saba ya ligi ya daraja la kwanza mfululizo.
Katika
Ligi ya Uingereza, ni klabu nne - Chelsea, Manchester City na Leicester
ambazo zimeshinda ligi katika misimu 12 iliopita.
Tangu
ianzishwa 1992 , ni klabu sita ambazo zimeshinda huku Blackburn Rovers
na Arsenal zikiwa klabu nyengine mbili zilizoshinda taji hilo.
chanzo:bbcswahili.com
No comments:
Post a Comment