MAMBO ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mfanyabiashara
maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kukiri
kuwa yeye ni changudoa mzee, kauli yake imeibua kimbembe.
KUPITIA SNAPCHAT
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Snapchat, mwishoni mwa wiki
iliyopita, Zari alitupia ujumbe akionesha kuwa yeye ni changudoa mzee,
lakini mwenye mafanikio akimjibu hasimu wake, mwanamitindo Hamisa Mobeto
bila kumtaja. “Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado
ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+, mama uliyeachwa mara mbili na
tuzo juu,” alisema Zari kupitia Snapchat. Kwa muda mrefu, Zari amekuwa
kwenye tifu la aina yake baada ya Mobeto kuzaa na bwana wake, msanii wa
Bongo Fleva miezi michache iliyopita.
KIBEMBE KILIVYOIBUKA
Kitendo cha Zari kutoa kauli hiyo, kimbembe kiliibuka mtandaoni mara
baada ya ukurasa wa Instagram wa Global Publisher, kutupia habari hiyo
ambapo wafausi wa mtandao huo walianza kurushiana maneno makali huku
kila mmoja akitoa msimamo wake.
AUNGWA MKONO, AKOSOLEWA
Kuna ambao waliunga mkono kauli hiyo kwa kile walichosema kwamba
aliandika kwa maana ya kumkejeli Mobeto, lakini si kwamba ni kweli yeye
ni changudoa, lakini wengine walicharuka na kusema kweli yeye ni
changudoa. “Jamani Zari siyo changudoa acheni kumshambulia kwa matusi.
Yule amesema vile kama kumkejeli Mobeto ambaye aliingia kwenye anga
zake, watu wengine sijui mkoje, mmekalia ujingaujinga tu,” alichangia
shabiki mmoja mtandaoni akimkingia kifua Zari.
Baada ya shabiki huyo kumtetea Zari, wengine waliibuka na
kumshambulia mama huyo wa watoto watano kwa kile walichosema kwamba
kweli mrembo huyo wa Uganda ni changudoa aliyejivisha ‘ngozi’ ya
ustarabu. “Acheni mambo ya kipuuzi…hivi mnafikiri Zari ana hela kama
inavyodaiwa? Yule ni changuduoa tu kama walivyo machangu wengine na kama
yeye mwenyewe alivyosema. Sema kinachompa hadhi yeye anajiuza kwa staha
tofauti na wenzake wanaojipanga barabarani.
UTAJIRI WAKE WAHUSISHWA
“Kule Sauz (Afrika Kusini) mnavyoona anaishi kwenye majumba ya
kifahari, anavyoonekana ana magari mapya kila siku mnafikiri yale ni
jasho lake? Uchangudoa tu ule ndiyo unaompa utajiri wote alionao, yule
msanii anajiona amepata kumbe amepatikana,” alisema shabiki huyo.
Mvutano huo ambao hadi tunakwenda mitamboni ulikuwa ukiendelea kwenye
ukurasa huo wa Global Publishers unaaongoza kwa kutembelewa na watu
wengi ndani na nje ya Bongo, ulisababisha watu kurushiana matusi ya
nguoni huku wengine wakienda mbali kwa kutaka kutafutana uso kwa uso,
nje ya mtandao huo wa Instagram ili wapeane ngumi kavukavu.
MWENYEWE AANIKA UKWELI
Baada ya kauli hiyo kuibua kimbembe, Zari amekuwa amewatolea uvivu
kwa kuonesha namna ambavyo ni mchapakazi kupitia ofisi zake mbalimbali
zinazomuingizia kipato halali tofauti na watu wanavyofikiri na kuweka
mawazo yao kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari amekuwa akionesha picha za
maduka yake ya nguo yaliyopo Afrika Kusini kwa kusindikiza na meseji
mbalimbali zinazoashiria kwamba yeye si mtu wa mchezomchezo linapokuja
suala la uwajibikaji. Ameonesha kwamba anatenga muda wake kwa kuwa bize
na kazi, lakini pia anatenga muda wake kwa ajili ya kufurahia maisha kwa
maana ya kuponda starehe katika viunga mbalimbali pande za Sauz na
nyumbani kwao, Uganda.
ANA VYUO SAUZ
Kama hiyo haitoshi, kupitia mahojiano yake ambayo yapo kwenye mtandao
wa Kijamii wa You Tube, Zari alifunguka kuwa anavyo vyuo vya urembo na
masuala ya ulinzi. Pamoja na hayo, amekuwa amekuwa akizungumzia
mafanikio mbalimbali anayoyapata kupitia matamasha yake makubwa hususan
lile la Zari All White Party ambalo linampa mkwanja mrefu kila mwaka.
Chanzo:globalpublisher.com
No comments:
Post a Comment