George Weah amezungumza kwa mara ya
kwanza tangu atangazwe Ijumaa kuwa mshindi wa kiti cha Urais nchini
Liberia katika uchaguzi wa marudio, amesema ataunda serikali ambayo
itajikita katika kuboresha maisha ya watu wa Liberia.
Weah ameahidi kuboresha maisha ya watu wa Liberia amesema ndicho kitakuwa kipaumbele chake cha kwanza atakapoingia madarakani mwezi Januari.
Weah ameahidi kuboresha maisha ya watu wa Liberia amesema ndicho kitakuwa kipaumbele chake cha kwanza atakapoingia madarakani mwezi Januari.
Katika hatua nyingine, mchezaji huyo wa
zamani wa mpira wa miguu, amesema wale wote wanaopenda kuwadanganya
watu kwa njia za rushwa hawatakuwa na nafasi katika serikali yake.
Weah amesema utawala wake utajengwa katika misingi ya kitaasisi kama alivyoanzisha Rais Ellen Johnson Sirleaf na amewaita raia wa Liberia walioko nchi za nje warejee kushuhudia maisha mapya na bora.
pia rais George Weah awataka raia wa Liberia walio nje kurudi kuijenga nchi.Rais mteule nchini Liberia,
George Weah amewashauri raia wa Liberia wanaoishi nchi za ng’ambo
kurudi nyumbani ili kusaidia kuijenga nchi yao.Weah amesema utawala wake utajengwa katika misingi ya kitaasisi kama alivyoanzisha Rais Ellen Johnson Sirleaf na amewaita raia wa Liberia walioko nchi za nje warejee kushuhudia maisha mapya na bora.
Nyota wa huyo zamani wa mpira wa miguu ambaye amechaguliwa kuwa Rais,
amesema hayo wakati wa mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu
atangazwe mshindi katika uchaguzi wa urais nchini humo.
Amesema ujuzi wa watu wa Liberia walio nchi za kigeni unahitajika kuijenga nchi hiyo.
Aidha, Rais Weah amepongezwa baada ya kusema kuwa ufisadi
hautavumiliwa katika utawala wake, ambapo Januari 2018 anaingia
madarakani rasmi.
No comments:
Post a Comment