Robert Mugabe.
ALIYEKUWA Rais wa Zambia na kuondolewa
madarakani hivi karibuni, Robert Mugabe, amepatiwa mafao kibao ya
kustaafu ambayo hutolewa na na serikali kwa viongozi wastaafu. Miongoni
mwa marupurupu yake ni pamoja na kupewa wasaidizi 20, usafiri wa ndege
na magari mbalimbali ya kumhudumia.
Hayo yamekuja baada ya kiongozi huyo
kuachia madaraka ambapo iliripotiwa kwamba pamoja na marupurupu mengine,
angepewa bonasi ya Dola milioni 10 (sawa na Sh. bilioni 22) Marupurupu
hayo yalitangazwa Jumatano wiki hii na Rais Emmerson Mnangagwa ambapo
watumishi wote 20 wa Mugabe wakiwemo walinzi sita, na gharama zote za
magari ya kifahari atakayopewa, yakiwemo aina ya Mercedes Benz S500,
yatagharimiwa na serikali.
Isitoshe, Mugabe na mke wake watapatiwa
pasipoti za kibalozi. Vilevile, wamepewa fursa ya kusafiri kwa ndege
mara nne kwa mwaka ndani na nje ya Zimbabwe kwa kutumia daraja la
kwanza. Watapewa pia makazi mahali popote katika Jiji la Harare, ambapo
samani na zana zote zinazohitajika na fedha za viburudisho zitalipwa na
serikali.
Mugabe ambaye alijiuzulu Novemba 21
mwaka huu baada ya chama chake kumfukuza na kuanza hatua za kumfungulia
mashitaka, amehakikishiwa pia kupata bima ya matibabu, mkewe na
wategemezi wake wote. Utawala wake uliochukua miaka 37 ulidaiwa kujaa
uvunjaji wa haki za binadamu, wizi wa kura na kuporomoka kwa uchumi hadi
pale Mnangawa alipochukua hatamu za uongozi. Hiyo ni baada ya Mugabe
kuungana na mkewe Grace (52) katika shutuma za kumpiga vita Mnangagwa.

No comments:
Post a Comment