Zlatan Ibrahimovic
KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho anaamini straika wake
Zlatan Ibrahimovic aliyerejea uwanjani hataweza kucheza vizuri kama
ilivyo-kuwa awali, hivyo yupo mbioni kumsajili Gareth Bale.
Kwa muda mrefu Mourinho amekuwa akihusishwa na mipango ya kumuhitaji
Bale kutoka Real Madrid ili akaongeze nguvu ya ushambuliaji katika
kikosi chake.
Gareth Bale.
Habari kutoka Man United, zimeeleza kuwa Mourinho anataka kumfanya
Bale kuwa usajili muhimu katika usajili ujao wa Januari ili kuimarisha
kikosi chake katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu England.
Awali, ilionekana kama ni vigumu kwa Bale raia wa Wales kutua Man
United lakini sasa inaonekana Madrid inaelekea kuchoka kuwa na
mshambuliaji huyo ambaye ana majeraha ya mara kwa mara.
Licha ya kuonekana kuwa na nia ya kumuuza, Madrid imeweka dau la
pauni milioni 79 kwa Bale japokuwa awali Man United inadaiwa kuweka
mkakati wa kutolipa zaidi ya pauni milioni 65 ili kumsajili Bale.
Tottenham Hotspur inaonekana kutaka kuizidi kete Man United, lakini
mazungumzo ya mwanzoni mwa msimu huu kati ya Bale na Man United yanampa
nafasi Mourinho ya kumnasa mchezaji huyo.
Mourinho anaelezwa kuweka presha ya kumsajili Bale kwa kiasi ambacho
Madrid watakitaka huku akibaki na mbadala wa Antonie Griezmann wa
Atletico Madrid endapo ishu ya Bale ikibuma.
Jumatano wiki hii, Bale aliifungia Madrid bao moja katika ushindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Al Jazira katika nusu fainali ya Klabu Bingwa ya
Dunia huko Falme za Kiarabu.
Madrid imepanga ikimuuza Bale iwasajili mmoja au wote kati ya Aubameyang, Dybala na Eden Hazard.
MANCHESTER, England


No comments:
Post a Comment