MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
anapaswa kutambua kuwa yeye kama Mkuu wa mkoa anajishughulisha na
matatizo ya watu hivyo kama hatabadili aina ya siasa azifanyazo basi
anapoteza muda wake kwa miaka yote mitano.
Gambo amesema kuwa yeye hana tatizo
lolote na Mbunge huyo wa Arusha mjini na kudai kuwa anapaswa kutambua na
kubadili aina ya siasa anazofanya kwa kuwa yeye amelenga kutatua
matatizo na changamoto za watu wa Arusha Mjini.
“Msuguano na Mbunge haupo lakini
anatakiwa tu asome alama za nyakati kwamba Mkuu wa Mkoa wa sasa
amedhamiria kuhangaika na shida za watu kama hatalitambua hilo atapoteza
muda wake kwa miaka yake yote mitano,” amesema Gambo.
Hata hivyo, Amesema kuwa yeye kama
kiongozi kijana anahitaji zaidi kukosolewa kuliko kusifiwa ili aweze
kujirekebisha sehemu ambayo ana mapungufu ili aweze kuwa kiongozi
madhubuti na mahiri zaidi.
No comments:
Post a Comment