Nairobi, Kenya. Kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)
nchini Kenya, Dk Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu nafasi yake katika
tume hiyo.
Dk Akombe ametuma taarifa ya kujiuzulu akiwa mjini New York nchini
Marekani anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa
kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.
Katika taarifa yake, Akombe amesema kwamba uchaguzi wa marudio wa
uraisi uliopangwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu haujafikia vigezo vya
kuwa uchaguzi huru na wa haki.
Akombe anajiondoa kwenye tume hiyo ya IEBC ikiwa imebaki wiki moja
uchaguzi wa urais kurudiwa kutokana na matokeo ya awali kufutwa na
mahakama kuu na kuamuru uchaguzi mpya ufanyike.
Agosti Akombe alizuiliwa kwenye uwanja wa ndege wa JKIA akielekea nchini Marekani.
Dk Roselyn Akombe Kwamboka alizaliwa 1976 katika kaunti ya Nyamira ,
na kusomea katika chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuelekea nchini
Marekani kwa masomo zaidi.
Ana shahada ya uzamifu katika masuala ya sayansi na kimataifa mbali
na shahada nyengine kama hiyo katika somo hilo kutoka chuo kikuu cha
Rutgers .
Hadi uteuzi wake katika tume hiyo alifanya kazi kama katibu katika
Umoja wa Mataifa mjini New York, wadhfa ambao anasema ulimwezesha kuwa
na uzoefu katika maswala
Uwezo wake mkuu amesema mbele ya kamati ya bunge nchini Kenya, ni
kutatua migogoro na kwamba ameishi ng’ambo kwa takriban miaka 15, hatua
iliomwezesha kuelewa zaidi mahitaji ya watu wanaoishi ughaibuni wakati
wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment