IEBC : UCHAGUZI WA MARUDIO KENYA KUFANYIKA OKTOBA 17 2017 - TANZA MEDIA ONLINE

Tuesday 5 September 2017

IEBC : UCHAGUZI WA MARUDIO KENYA KUFANYIKA OKTOBA 17 2017



Baada ya siku tatu kupita toka Mahakama ya juu nchini Kenya itangaze kufuta matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Kenya uliyofanyika August 8 2017 na Rais Uhuru Kenyata kufanikiwa kuibuka mshindi mbele ya Raila Odinga, leo tume ya uchaguzi Kenya IEBC imetangaza tarehe ya uchaguzi mpya wa marudiano.

Kwa mujibu wa katiba ya Kenya matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Kenya baada ya kutangazwa kufutwa na Mahakama ya juu, sheria au katiba ya Kenya inataka uchaguzi Mkuu kurudiwa ndani ya siku 60, hivyo leo tume ya uchaguzi Kenya IEBC imetangaza kuwa October 17 2017 ndio tarehe ya uchaguzi wa marudio.

No comments:

Post a Comment