Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi mkuu wa TFF Revocatus Kuuli amemtangaza
Wallace Karia kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kufuatia uchaguzi wa shirikisho hilo uliofanyika leo Makao Makuu ya
Tanzania Dodoma.
Wallace Karia ameibuka mshindi wa nafasi ya Urais wa shirikisho hilo huku nafasi ya Makamu ya Rais ikichukuliwa na Michael Wambura, kwa matokeo hayo Wallice Karia anakuwa mrithi wa aliyekuwa Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Jamal Malinzi

Wallace Karia (kulia) akiwa na makamu wake Michael Richard Wambura
Baada ya kutangazwa washindi viongozi hao waliweza kula kiapo mbele ya
wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi, naa baada ya hapo Rais mpya wa shirikisho
la mpira wa miguu (TFF) Wallace Karia aliwashukuru wajumbe na
watanzania kujumla na kusema kuwa furaha aliyonayo iende kuwa furaha ya
kazi kwa kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya soka la Tanzania.
Hata hivyo Wallace amesema katika uongozi wake uwazi na uwajibikaji ndiyo nguzo kuu na kusema hivi sasa ubabaishaji katika mpira wa miguu sasa umekwisha, ubabaishaji wa soka sasa ni mwisho.
Katika uchaguzi huo wajumbe wa Kamati Kuu ya Uchaguzi waliweza kuchagua pia Kamati ya Utendaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) katika kanda mbalimbali mbao ni

UONGOZI MPYA TFF NI KAMA IFUATAVYO:
NAFASI YA RAIS
Wallace Karia
Makamu wa Rais
Michael Wambura
Kanda namba 13 -Dar es Salaam
Mshindi ni Lameck Nyambaya
Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga
Mshindi ni Khalid Andallah
Kanda No 11 Pwani na Morogoro
Francis ni Ndulane ameshinda
Kanda Namba 10 (Dodoma na Singida)
Mshindi: Mohamed Abeid
Kanda Namba 9 (Lindi na Mtwara)
Mshindi: Dunstan Mkundi
Kanda namba 8 (Njombe na Ruvuma)
Mshindi: James Mhagama
Kanda namba 7 (Mbeya na Iringa)
Mshindi: Elias Mwanjala
Kanda Namba 6 (Katavi na Rukwa)
Kenneth Pesambili
Kanda namba 5 (Kigoma na Tabora)
Issa Bukuku
Kanda namba 4 (Arusha na Manyara)
Mshindi: Sarah Chao
Kanda namba 3 (Shinyanga, Simiyu)
Mshindi: Mbasha Matutu
Kanda namba 2 (Mara, Mwanza)
Mshindi: Vedastus Lufano
Kanda namba 1 (Kagera, Geita)
Mshindi: Salum Chama
No comments:
Post a Comment