Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza kwamba wananchi wote
wanaofika katika vituo vya afya vya serikali wapimwe virusi vya Ukimwi
kwa lazima, wapatiwe ushauri nasaha na tiba.
Rais Lungu amesema, sera hiyo mpya inaenda sawia na agenda ya
serikali ya kutokomeza virusi vya HIV nchini humo ifikapo mwaka 2030.
Katika tangazo hilo, kiongozi huyo amesisitiza umuhimu wa kulinda
maisha ya wale walioathirika na wale ambao wako hatarini kuambukizwa
virusi hivyo.
Amesema, licha ya sera hiyo kukiuka haki ya mtu kupima kwa hiari
lakini akasisitiza kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kuweka rehani maisha
ya binadamu mwenzake.
Sera hiyo inakiuka muongozo wa Shirika la Afya Duniani, WHO, na
Shirika la Ukimwi la Umoja wa Mataifa, UNAIDS, unaohamasisha watu kupima
Vvu na kupata ushauri nasaha kwa hiari.
No comments:
Post a Comment