Polisi wamtia nguvuni kiongozi UVCCM Arusha aliyejifanya Afisa Usalama wa Taifa - TANZA MEDIA ONLINE

Friday, 11 August 2017

Polisi wamtia nguvuni kiongozi UVCCM Arusha aliyejifanya Afisa Usalama wa Taifa

Polisi Mkoa wa Arusha inamshikilia Diwani wa Kata ya Sambasha (CCM) iliyopo Wilayani Arusha Vijijini Lengai Ole Sabaya kwa kosa la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa.


Sabaya ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Arusha amekamatwa tena na jeshi la polisi na kutakiwa kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kufuatia kufutwa kwa kesi yake ya awali ya kujifanya ni Afisa wa Usalama wa Taifa (TISS).

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema ni kweli wanamshikilia Sabaya kwa kosa hilo hilo la kujifanya afisa wa idara ya usalama.

Mkumbo amesema awali alipoachiwa mahakamani polisi waliendelea na upelelezi wa kesi yake na kudai hivi sasa atapelekwa tena mahakamani muda wowote kujibu tuhuma zinazomkabili ikiwa pamoja na kujifanya Afisa Usalama wa Taifa (TISS) lakini pia kughushi kitambulisho cha Usalama wa Taifa.



Lengai Ole Sabaya mwaka jana alifikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashitaka mawili ambapo la kwanza ni kuwa Mei 18 mwaka 2016, katika Hotel ya Sky Motel, Mshitakiwa Sabaya alijifanya Afisa usalama wa Taifa (TISS) na kupata huduma ya kulala katika hotel hiyo, kwa kupata chakula na vinywaji wakati siyo kweli.

Lakini alishitkiwa kwa kosa la pili la kughushi kitambulisho cha TISS kilichosomeka MT.86117 wakati akijuwa wazi kuwa kufanya hivyo
ni kosa kisheria

No comments:

Post a Comment