HAWA NDIO WALIOHUSIKA KWENYE KIFO CHA 2PAC PIA NOTORIOUS BIG - TANZA MEDIA ONLINE

Friday 5 February 2016

HAWA NDIO WALIOHUSIKA KWENYE KIFO CHA 2PAC PIA NOTORIOUS BIG


Featured-2pac-Vs-Biggie

Aliyekuwa askari wa LAPD detective Greg Kading ameongea na HipHopDX nakusema “Kesi ya vifo vya 2 Pac na BIG haiwezi kwenda mahakamani sababu mashahidi na watuhumiwa wengi wamesha fariki“
Waliohusika kwenye mauwaji ya wasanii Biggie na Tupac wametajwa kwenye filamu hii ya Murder Rap: Inside The Biggie & Tupac Murders iliyotoka February 1 2016.
Filamu inaonyesha kazi alizofanya aliyekuwa polisi na mpelelezi wa LAPD Greg Kading, aliyekuwa na askari wake wakichunguza na kupeleleza mauwaji hayo.
Kading anasema “Rapa Puff Daddy aliajiri member wa kundi la Crips Duane Keith “Keffe D” Davis kumuuwa 2 Pac Shakur na Suge Knight, pesa ya kazi hii ilikuwa dola milioni $1zakimarekani, binamu wa Keffe D amabye ni Orlando “Baby Lane” Anderson ndiye aliyempiga risasi  Tupac mjini Las Vegas mnamo September 7, 1996, 2 Pac alifariki siku tano baadae September 13“
Kading anasema Suge Knight alimpa kazi member wa kundi la Bloods Wardell “Poochie” Fouse kumuwa The Notorious B.I.G. kama kulipiza kisasi kwa kifo cha 2 Pac. Biggie Smalls alipigwa risasi Los Angles March 9, 1997.
Haya ni maelezo ya polisi aliyechunguza kesi hii.

No comments:

Post a Comment