Barua ya Jack Cliff toka gerezani China. - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 17 February 2016

Barua ya Jack Cliff toka gerezani China.



jacck
Mwanadada Mtanzania Jack Cliff ambaye kwa sasa yuko gerezani Macau China kwa kosa la kujaribu kuingiza dawa za kulevya nchini humo ameandika barua ya wazi kwa mtangazaji Millard Ayo na kuomba isomwe kwa watu wote.
Mwadada huyo ambaye aliwahi kuwa video vixen (video queen) kwenye video za bongo fleva na mpenzi wa zamani wa msanii Jux amekiri kwenye barua hiyo kuwa amepatikana na hatia hizo na kuomba msamaha kwa wale wote wanaompenda kwa kuwaangusha.
Pia Jack ameweka wazi kuwa bado yuko jela na amepewa miaka kadhaa ya kutumikia,hakuiweka wazi na kuongeza kwa kusema kuwa hafurahii hali iliyopo pia hawezi kujutia wala kumlaumu yeyote kwa kilichotokea bali amejifunza kujitambua upya kwani alishapotea kitambo.
Lakini pia Jack amewataka watanzania kutoamini kila kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu yeye,vingine sio vya kweli na kuwaomba wasimhukumu kwa kuwa bado hawajisikia chochote kutoka kwake.
Kwa hatua nyingine Jack amefunguka kuhusiana na mpenzi wake wa zamani Jux na kueleza jinsi gani amem miss na kumwomba msahama kwa kumuumiza na pia kumtakia kheri kwenye mapenzi yake mapya.
Kuhusiana na watu wanaomsaidia Jack amesema familia yake pekee ndio imekuwa ikimsaidia kwa kiwango kikubwa na kuwashukuru wote waliokwenda kwenda kumuona ikiwemo Mtanzania Athumani maarufu kama wabogoyo ambaye amekuwa akimtembelea kila wiki.Aidha Jack amemshukuru mpenzi wake wa zamani anayeanziwa na heruf H kwa kuwa pamoja naye na kuwashukuru marafiki wake ambao ni Martin Kadinda,Imelda na Myla kwa kutoa muda wao.
Jack amemalizia kwa kusema kuwa yeye sio wa kwanza wala wa mwisho kukamatwa kwa kosa hilo hivyo atashukuru kwa yeyote atakayemwombea na hatajali kwa watakaomsema vibaya kwani hafanyi kitu kumpendezesha yeyote yule.

No comments:

Post a Comment