TEAM YA MAANDALIZI YA “LADY IN REDY 2016″ YAKUTANA NA WANAHABARI LEO DANKEN HOUSE - TANZA MEDIA ONLINE

Saturday 30 January 2016

TEAM YA MAANDALIZI YA “LADY IN REDY 2016″ YAKUTANA NA WANAHABARI LEO DANKEN HOUSE

Team ya maandalizi ya Fashion Show maarufu kama “Lady In Red 2016″imekutana na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa “Danken House” kujadili na kutoa hamasa kwa Designers na wadau mbalimbalia ambao pia ni wapenzi wa mitindo.
Uongozi huo ambao unasimamiwa na Mama wa Mitindo ambaye anajulikana kama “Asya Idarous”  umesema kuwa “Jukwaa la “Lady In Red 2016″ litakuwa la ainayake kufuatia jitihada na juhudi zinazofanywa na walengwa wa tukio hilo, ambalo linategemea kupandisha Designers wengi zaidi hapa nchini siku ya Jumapili 31/1/2016 katika ukumbi wa Danken House.
Miongoni kati ya Designers watakao panda kwenye Stage siku hiyo ni Bemy Masai, Kelly Peter, Faustin Simon, Mtetesi Forcus, Barnabas, Mwanahamisis Kiroho, Nelson Thomas, Walter Demarian, Dorine Lymo, Evemary Sospeter, Fatma Rashid, Samweli Zebedayo, Kulwa Mkwandule, Jocktan Makeke, Saleem Siwila, Love Delamo, Abdul Mwene, Karol Mngumbi Jay Julius, Furaha, Joshua, Benja, Lili, Veronica, Rukia Walele nk.
Hivyo kama nawewe ni mpenzi wa mitindo usikubali kupitwa na tukio hilo, kiingilio ni buku 10000/= na viti vya mbele ni 30000/= Nyote mnakaribishwa ulisema oungozi wa maandalizi ya Tukio hilo.

DSCN9613 DSCN9616 DSCN9618 DSCN9620 DSCN9621 DSCN9622 DSCN9623 DSCN9624 DSCN9625 DSCN9650 DSCN9652 DSCN9656 DSCN9657
Picha za Pamoja za Designers mara baada ya kumaliza mazungumzo ya “Lady In Red 2016″ na waandishi wa Habari leo.

No comments:

Post a Comment