LIST YA WASANII WA HIP HOP WAKIMAREKANI WASIOTUKANA KWENYE NYIMBO ZAO - TANZA MEDIA ONLINE

Saturday 23 January 2016

LIST YA WASANII WA HIP HOP WAKIMAREKANI WASIOTUKANA KWENYE NYIMBO ZAO


Ukweli ni kuwa ili kuwa na wimbo wa rap/hiphop usioboa ni lazima tuwape nafasi wasanii kufanya sanaa yao bila mipaka.Baadhi ya wasanii wasiotukana ndani ya nyimbo zao kutoka Marekani ni hawa…
  1. Smith 
  2. Common 
  3. Flo Rida 
  4. OutKast 
  5. PitBut 
  6. Chamillionaire 
  7. LL Cool J 
  8. Rakim 
  9. Lupe Fiasco 


 
HIPHOP

 NA HIZI NDIO SABABU KUU ZA WASANII WENGI MAREKANI KUTUKANA KWENYE NYIMBO ZAO
 
1] Maisha wanayotoka baadhi ya wasanii wa rap yana changia hasira kwenye mashairi yao, maisha ya umasikini,fujo, kuishi bila matumaini. mashairi makanli na kutojali kuyasema yanatokana na hasira za maisha yao ya nyuma.

2] Kana wimbo wa Kanye na Jay Z ‘Niggas In Paris’ ulivyosema “it’s provocative, it gets the people going.” Raia wanapenda mambo kama hayo,yanaonyesha kutojali na kuchangamsha mawazo ya msikilizaji.

3] Kufikisha ujumbe kwa nguvu zote, inasemekana unapotukana katikati ya sentesi fulani inaonyesha umeweka msisitizo zaidi kwenye kauli hio yenye matusi au maneno makali. Ila sio lazima kutukana ili uwe rapa mzuri na kufikisha ujumbe wako.

4] Freedom Of Speech pia ni miongoni mwa sababu zinazochangia msanii kuwa huru kusema chochote kwneye muziki wake. Hii ni haki ya kila raia kutoa maoni yake anavyojiskia.

5] Ubabe, Msanii wa rap/hiphop ni muhimu kuonyesha jamii kuwa unauwezo kuwa kushawishi na kufanya jambo sababu ya nguvu zako,kumiliki jambo lolote utakavyo, kuwa mbabe kwa washindani wenzako kwenye muziki huu, matusi na maneno makali husaidia kufiisha ujumbe huo, matusi huonyesha hujali kama watakasirika na kwamba hawakuwezi.

6] Mziki unachangamsha, ni rahisi kusema hatutaki matusi kwenye muziki na kuweka Beep kwenye kila tusi ila tafakari,je unapenda kusikia matusi na maneno makali yote kwenye wimb na jinsi yanavyo tamka kwa mikogo ya kisanii au tuyatoe kabisa ?

No comments:

Post a Comment