Katibu
Mkuu Yanga, Dk Jonas Tiboroha ameambiwa kuchagua moja, kujiuzulu au
afukuzwe kazi. Yeye ameamua kubwana manyanga na barua atakabidhi leo,
rasmi.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza Dk Tiboroha ametakiwa
kufanya hivyo baada ya kugundulika kulikuwa na madudu kibao wakati wa
uongozi wake.
Imeelezwa,
hiyo imetokana na kamati ya utendaji na uongozi wa juu wa Yanga
kugundua kulikuwa na tatizo na mambo hayakwenda kama ilivyotakiwa kwa
kufuata taratibu za kiungozi.
“Unajua
Tiboroha ameharibu mambo mengi sana, lakini mwisho wake umekuwa ndiyo
huo. Uongozi umekuwa mvumilivu sana na watu hawakujua tua.
“Lakini mwisho imegundulika kuna mambo kadhaa ambayo yalikiuka sababu za kiungozi na hayakuwa sawa.
“Kamati
ya utendaji pia imeridhia hilo baada ya kufanya uchunguzi wa kina na
kulibaini suala hilo,” kilieleza chanzo cha uhakika," kilieleza chanzo.
Lakini taarifa nyingine zinahusisha figisu ya masuala ya haki, unyoofu wa mambo katika masuala kadhaa na blogu hii inaendelea kufuatilia ili kupata uhakika kilichosababisha uongozi huo wa Yanga kufikia uamuzi huo na pia kuamua kumpa nafasi ya kujiuzulu mwenyewe au afukuzwe."
Juhudi za kumpata Dk Tiboroha katika simu kuanzia leo saa moja asubuhi hazikuzaa matunda kutokana na kuonekana simu yake ilikuwa imezimwa muda wote.

No comments:
Post a Comment