Winnie Mandela, mke
wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa
ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81.Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.
Winnie
alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe - Nelson
Mandela - walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela
kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw
Mandela.
Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27.Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata.Msemaji
wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa: "Amefariki
baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka
hospitalini mara kwa mara tangu mwnazo wa mwaka.
"Alifariki kwa amani mapema Jumatatu adhuhuri akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake."
Askofu
mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama "ishara
kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi," kwa mujibu wa AFP.Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa.Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa.
Katika
kipindi chote cha miaka 27 mumewe alipokuwa gerezani bila matumaini ya
kuachiwa huru kutokana na hukumu ya kifungo cha maisha jela alichopewa
mwaka 1964, Bi Winnie alilazimika kubeba jukumu la ulezi wa watoto na
pia kuendeleza kampeni za kisiasa kutaka mashujaa wa kupigania nchi yao
waachiwe huru hasa mumewe.
"Kamwe hatutapoteza matumaini na watu
wangu hawatapoteza matumaini kamwe, bila shaka tunatarajia kwamba kazi
itaendelea," alisema wakati huo.Kutokana na hayo Bi Winnie
Mandela alilazimishwa kusalia tu huko Brandford katika jimbo lao la
Orange Free katika miaka ya 70 baada ya operesheni mojawapo za kupambana
na ubaguzi wa rangi zilizokuja kujulikana zaidi kama the Soweto
Uprising.
Kama ilivyomtokea mumewe, Bi Winnie alifungwa
gerezani, na hata kuwekwa katika kizuizi cha pekee yake ambacho ni
mojawapo ya vifungo vigumu zaidi gerezani vinavyowaathiri wafungwa
kisaikolojia.Lakini baada ya kuachiwa kwake mtindo wa mapambano
yake dhidi ya ubaguzi wa rangi ulianza kupata sifa mbaya hasa pale
alipoonekana kuendekeza tabia ya kuwavisha tairi shingoni wale
waliolengwa kwa tuhuma za usaliti na kisha kuwachoma moto.
"Kwa 'mikufu yetu' tutaikomboa nchi hii," alizoea kusema.
Mambo
yalizidi kumwendea mrama kutokana na matendo ya baadhi ya walinzi wake
katika kile kikundi kilijulikana kama the Mandela United Football Club.Walipatikana
kuhusika katika kitendo cha kumteka nyara na kumuua kijana mmoja
mwenye umri wa miaka 14 aitwae Stompie Moeketsi -kwa tuhuma za kwamba
alikuwa akitoa siri kwa maadui zao.
Japo Bi Winnie Mandela
aliepuka hukumu ya kifungo jela - baadaye tume ya ukweli na maridhiano
iliyoongozwa na askofu Desmond Tutu, iliyokuwa inachunguza ukweli kuhusu
matendo tata katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na kutafuta
maridhiano, ilimpata Bi Mandela na hatia ya kutowajibika kisiasa wala
kimaadili wakati wa kitendo hicho.
Licha ya misukosuko hiyo Bi Mandela alibaki kuwa
mtu muhimu sana katika siasa za Afrika kusini na kuwa mwakilishi muhimu
waa wanawake waliopambana kufa na kupona dhidi ya utawala wa ubaguzi wa
rangi uliokuwa unaendelezwa na Wazungu walio wachache nchini humo.
Katika
siku za baada ya uhuru wa Afrika Kusini anakumbukwa zaidi kwa kuwa
miongoni mwa wachache katika uongozi wa ANC waliomuunga mkono aliyekuwa
rais wa Afrika Kusini Thabo mbeki katika kushtumu na kulaani vikali
vitendo vya kuwashambulia wahamiaji wa Kiafrika huko nchini Afrika
Kusini.
KUSINI - mashambulio yaliyobadikwa jina xenophobic
attack. Pia amekuwa muungaji mkono mkubwa wa kiongozi wa chama cha
Economic Freedom Fighters CHA Julius Malema , kilichojimegua kutoka ANC
ambacho kilimkosoa vikali rais aliyelazimika kung'atuka Jacob Zuma.
Historia
ya Bi Winnie Madikizela Mandela, hadi kifo chake inabaki akikumbukwa
zaidi kama mama wa taifa la Afrika kusini aliyesimama kidete dhidi ya
ubaguzi wa rangi katika umri wake wote.
chanzo;bbcswahili.com
No comments:
Post a Comment