WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji kuaga miili ya
askari 14 waliouawa na waasi wa ADF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC) ambapo shughuli ya kuaga miili ya askari hao imefanyika leo
Alhamisi, Desemba 14, 2017 katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa, Upanga jijini Dar es Salaam.
Viongozi wengine waliohudhuria katika kuaga miili hiyo ni Rais
Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, wakuu komandi za anga, maji, nchi kavu
na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), viongozi wa Umoja wa Mataifa, na wakuu
wa vyombo vya ulinzi na usalama, askari na wananchi.
Akizungumza wakati wa shughuli ya kuaga miili hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema;
“Kidiplomasia tunatumia nafasi hii kwenda kusaidia mataifa ya wenzetu
ndio maana tumeshiriki katika vita za ukombozi kwenye nchi kadhaa za
Kusini mwa Afrika, pia shughuli za kulinda amani katika nchi mbalimbali.
“Hivi sasa jeshi letu linaendelea na shughuli hizo nchini Lebanon,
Dafur na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na katika nchi zote hizo
maaskari wetu wanasifiwa kwa uvumilivu, uhodari wa kazi, na nidhamu ya
hali ya juu,” alisema Majaliwa.
Baada kukamilika shughuli ya kuaga miili hiyo itasafirishwa kwao mazishi.
No comments:
Post a Comment