Mipasho! Mwanamitindo mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari The
BossyLady’ ambaye aliingia katika mtafaruku wa maisha yake ya kimapenzi,
kwa mara nyingine juzikati alionyesha kuwepo kwa kutoelewana kwao baada
ya kuliamsha dude kwa kutoa maneno ya kumnanga mzazi mwenzake.
Awali, vyanzo vyetu vilivyo karibu na mrembo huyo mwenye watoto
watano, alisema kwa sasa hana uhusiano mzuri na baba wa watoto wake
wawili, kwa kile kinachosemwa kuwa ni kitendo cha mwenzake huyo
kuendekeza mapenzi na wanawake wengine.
“Ni kama mchezo unaelekea mwishoni hivi sasa, maana maneno na ugomvi
kati yao hauishi, jamaa anafanya kazi kubwa kuficha kuhusu huu uhusiano
wake kuwa juu ya mawe, lakini ukweli ni kwamba hakuna dalili za wawili
hawa kukaa tena imara kama zamani,” kilisema chanzo hicho.
Katika tukio la hivi karibuni, mwanamama huyo aliandika katika
mtandao wake maneno yenye kumlenga mzazi mwenzake, akisema anaendekeza
wanawake na watoto wengi na kwamba badala ya kuona anauza kazi zake
nyingi za muziki, yeye amekuwa hodari wa eneo ambalo hahusiki.
Katika kumnanga huko, Zari alisema endapo mtu anatafuta ubalozi wa
kondom, ambacho ni kifaa cha kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukizwa
kupitia ufanyaji mapenzi, basi hana haja ya kuhangaika kumpata, kwa kuwa
tayari mtu.
No comments:
Post a Comment