Kiongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa, Raila Odinga amedai atakula kiapo kama “rais wa watu” Desemba 12.
Akiwahutubia wafuasi wake katika barabara ya Mayanja baada ya
kutawanywa na polisi kwenye viwanja vya Jacaranda, alisema atatumia
Ibara ya 1 kuapa inayosema mamlaka ya nchi yanatoka kwa watu.
“Mimi si mwoga. Mimi nitaapishwa Siku ya Jamhuri, mimi ndiye rais
halali,” alisema akijibu malalamiko ya wafuasi wake waliosikia awali
akisema hawezi kula kiapo ili asichafue taswira yake kimataifa.
Awali mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa
Jacaranda ili kuomboleza watu waliouawa na polisi hivi karibuni
ulisambaratishwa na polisi.
Polisi kuanzia mapema asubuhi walifunga eneo lote la Jacaranda ambako
ingefanyika misa hiyo ya kumbukumbu sambamba na tukio la Rais Uhuru
Kenyatta kuapishwa kuongoza muhula wa pili wa miaka mitano baada ya
kushinda uchaguzi wa marudio Oktoba 26.
Magari makubwa ya polisi yalionekana yakiranda eneo hilo na watu waliojikusanya walitawanywa kwa mabomu ya machozi.
Baadaye Nasa walijikusanya barabara ya Mayanja.
Baadaye Nasa walijikusanya barabara ya Mayanja.
No comments:
Post a Comment