Aliyekuwa Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Dkt. Wilbroad Slaa amezungumzia hatua aliyoichukua Rais John Magufuli
kumteua kuwa Balozi.
Dkt. Slaa amesema ubalozi ni nafasi ambazo zipo katika himaya ya Mkuu wa Nchi hivyo bila shaka hadi Rais kufikia hatua ya kumteua atakuwa na sababu za uteuzi huo.
“Hatimaye kama ni mapenzi wa Mungu namshukuru kwa uteuzi huo ninachoweza kusema katika hatua hii ni kwamba ni wajibu mkubwa katika kipindi hiki cha kujenga taifa letu. Kama ni kutoa mchango wangu nitakuwa tayari kutoa, Mwenyenzi Mungu akinisaidia” Dkt. Slaa amekiambia kituo cha runinga cha Azam.
Hapo juzi November 23, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Magufuli alimteua Dkt. Wilbroad Slaa kuwa Balozi na inatarajiwa ataapishwa pindi taratibu zikikamilika.

No comments:
Post a Comment