MTANZANIA ABDI BANDA AANZA VYEMA LIGU KUU SOUTH AFRICA - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 23 August 2017

MTANZANIA ABDI BANDA AANZA VYEMA LIGU KUU SOUTH AFRICA

Image result for abdi banda
Abdi Banda
BEKI Mtanzania, Abdi Hassan Banda leo ameinusuru timu yake mpya, Baroka FC kulala nyumbani mbele ya Orlando Pirates ya kocha Mganda, Milutin Sredojevic ‘Micho’ baada ya kuifungia bao la kusawazisha katika sare ya 1-1.
  Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini uliofanyika Uwanja wa Peter Mokaba mjini Johannesburg, Banda aliyejiunga na timu hiyo mwezi Juni akitokea Simba ya Tanzania, alifunga bao hilo dakika ya 73 kwa kichwa kufuatia mpira wa kona ya juu juu.

Baroka FC waliokuwa nyumbani, walikubali kuruhusu bao katika dakika ya 41 baada ya Thabo Qalinge kuinfungia Orlando bao la kwanza. 
 
Vigogo hao chini ya Mserbia, Micho walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0, ikionekana kama wana nafasi ya kuongeza bao la pili katika kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment