MGOMO WA MADEREVA 2000 WASITISHWA - TANZA MEDIA ONLINE

Monday 21 August 2017

MGOMO WA MADEREVA 2000 WASITISHWA

Ule mgogoro ulioibuka mapema leo asubuhi pale stendi ya daladala simu 2000,umeisha baada ya meya wa manispaa ya ubungo kuingilia kati.
Taarifa aliyotoa kiongozi huyo hivi punde imesisitiza pia kuwachukulia hatua waliohusika kuanzisha mgogoro huo.

 HII NDIO TAARIFA KAMILI  YA MH BONNIFACE- MEYA WA UBUNGO

Watendaji wachache wa halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wametia dosari jina Halmashauri kwa Uzembe na Kutokujua sheria.

Kwamba Leo wameamka na Kuongeza Ushuru kutoka kiasi cha shillingi 500 mpaka 1000,bila kujua kuwa Sheria hairuhusu jambo Hilo.

Tumeagiza kurudi kiasi kilekile cha shillingi 500 kwa siku kwa kila daladala,kwakuwa Baraza la Madiwani halikuongeza kiasi hicho kama inavyotakiwa na Sheria,
na Baadae Mabadiliko hayo kusainiwa na Waziri Mwenye Dhamana na TAMISEMI, ndiyo ianze kutumika.
Lakini hakuna Maombi ya Namna hiyo taliyotolewa na Baraza la Madiwani na Hakuna Waziri aliyeruhusu jambo hilo.

Kama Meya wa Halmashauri ya Manispaa ubungo,nimesikitishwa na Watendaji wetu wa Halamshauri kutuingiza kwenye Mgogoro na Watumiaji wa Hiduma hii bila sababu za Msingi,Tunasubiria vikao tuh kuchukua hatua kali za Kinidhamu kwa mujibu wa  kisheria.

Aidha kuhusu Baraara ya simu 2000 kuwa Mbovu,nimeelezea kuwa hiyo barabara pesa zake zimezuiwa kwa sababu za kisiasa,Lakini pesa hizo zipo tangu 2015, kiasi cha shillingi Billioni 1.7  kutoka BENKI YA DUNIA,pamoja na Wizara ya fedha kuzuia fedha za fidia ndicho kinacho chelewesha barabara kuendelea kuwa Mbovu

MWISHO
Hatua kali za kinidhamu kwa waliopandisha Ushuru kinyume na Sheria inavyotaka;kwa Madiwani kukaa na kupanga na kisha waziri kupitisha zitachukuliwa kwa waliohusika,na Kero ndogondogo za stendi kama walinzi na wahudumu wa vyoo pia zita shughulikiwa HARAKA SANA.

Boniface Jacob
Mstahiki Meya
Manispaa ya Ubungo

*Senior councilor Ubungo.*

No comments:

Post a Comment