NDANDA YAPELEKA SHANGWE MSIMBAZI NA JANGWANI - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 6 April 2016

NDANDA YAPELEKA SHANGWE MSIMBAZI NA JANGWANI


Ndanda FC
Ndanda FC ya mkoani Mtwara imeikazia Azam FC na kuilazimisha sare ya kufungana magoli 2-2 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliosukumwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Azam walianza kupata bao dakika ya 16 kipindi cha kwanza kupitia kwa Ramadhani Singano ambaye aliunganisha pasi ya Michael Balou kabla ya Didier Kavumbagu kutupia kambani bao la pili muda mfupi kabla ya kwenda mapumziko.
Atupele Green alizifungua nyavu za Azam kwa kuusukuma mpira kambani kwa mkwaju wa penati baada ya golikipa wa Azam Aishi Manula kumwanusha Paul Ngalema kwenye eneo la hatari wakati akijaribu kuokoa hatari golini kwakwe.
Bao la kusawazisha la Ndanda FC lilikuwa ni la kujifunga ambapo beki wa Azam FC Agrey Morris aliugonga mpira uliokuwa unaelekea goli na kuubadilisha mwelekeo kisha kumshinda golikipa Aishi Manula na kuzama wavuni.
Matokeo hayo ni habari njema kwa Yanga na Simba ambazo timu zote hizo tatu zinaongoza mbio za kuwania ubingwa wa ligi msimu huu.
Takwimu muhimu
  • Metokeo ya mabao 2-2 kati ya Azam FC dhidi ya Ndanda FC ni sare ya kwanza katika mechi nne zilizovikutanisha vilabu hivi. Mechi tatu zilizopita zimeshuhudiwa Azam aikiibuka na ushindi mara mbili wakati Ndanda ikipata ushindi kwenye mchezo mmoja.
  • Mabao manne kufungwa kwenye mchezo mmoja (Azam 2-2 Ndanda) ni mabao mengi kufungwa kwenye mechi zilizozikutanisha Azam na Ndanda.
  • Sare ya mchezo wa leo unaifanya Ndanda kupata matokeo ya sare kwenye mechi 12 wakati Azam wao ni sare yao ya saba kwenye mechi za ligi. Timu zote (Azam na Ndanda) hii ni sare yao ya pili mfululizo, Azam ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Toto Africans uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza huku Ndanda yenyewe ikitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Tanzania Prisons.
  • Azam imefikisha pointi 52 pointi 5 nyuma ya vinara Simba na pointi moja nyuma ya Yanga baada ya kucheza michezo 23 Simba imeshacheza mechi 24 wakati huo Yanga yenyewe ikiwa imeshuka uwanjani mara 22. Ndanda inafikisha pointi pointi 27 na kujikita kwenye nafasi ya tisa.

No comments:

Post a Comment