MWENYEKITI
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba
anajitolea kuijenga Uwanja wa mazoezi klabu hiyo kwa mapenzi yake.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE, Hans Poppe amesema kwamba amekuwa
akiumia sana kuona Simba SC inahangaikia Uwanja wa kufanyia mazoezi
wakati tayari ina eneo lake Bunju.
“Nilikaa
nikatafakari gharama za ujezi wa Uwanja mzuri wa mazoezi, nikaona
ninaweza kuifanyia kitu hiki klabu yangu. Na sasa nipo katika mchakato
wa kuanza ujenzi muda si mrefu,”amesema Poppe.
Kapteni
huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba
anataka Simba SC iondokane kabisa na tatizo la Uwanja wa mazoezi.
“Sitapenda
kuendelea kuona tunahangaikia Uwanja wa mazoezi, ndiyo maana nimeamua
kujitolea kwa mapenzi yangu kuwajengea Uwanja wa mazoezi,”amesema.
Pamoja
na hayo, Poppe ameipongeza Serikali kwa kumpa zawadi ya kiwanja,
mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mbwana Samatta baada ya kushinda
tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.
“Nichukue
fursa hii pia kuipongeza Serikali kwa kumpa Samatta kiwanja baada ya
heshima kubwa aliyoiletea Tanzania, nasikia wamempa na fedha pia. Ni
vizuri sana. Na ninadhani hii itawaamsha na wachezaji wengine waongeze
bidii,”amesema.
Juzi,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
alimkabidhi Samatta anayechezea TP Mazembe ya DRC hati ya kiwanja
kilichopo eneo la Kigamboni, Dar es Salaam pamoja na bahasha ya fedha,
ambazo hata hivyo kiwango chake hakikutajwa.
Kwa
sasa Samatta yuko mbioni kujiunga na klabu ya KRC Genk ya Ligi Kuu ya
Ubelgiji na tayati Ubalozi wa nchi hiyo hapa Tanzania umempatia viza ya
kwenda huko kukamilisha usajili wake.
Samatta akiwa na bahasha ya burungutu la fedha alilokabidhiwa na Waziri wa Nyumba Ardhi na Maendelea Wiliam Lukuvi (kushoto) pamoja na hati ya kiwanja (katikati) ni Waziri wa Habari na Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye
Ingawa bado klabu yake, TP Mazembe haijatangaza rasmi, lakini taarifa zinasema mwishoni mwa mwaka jana, Rais wa klabu hiyo ya Lubumbashi, Moise Katumbi alifikia makubaliano na klabu hiyo ya Ubelgiji juu ya biashara ya mchezaji huyo. Samatta aliyejiunga na TPM mwaka 2011 akitokea Simba SC aliyoichezea kwa nusu msimu, akitokea African Lyon, anaondoka Mazembe baada ya kuichezea mechi 103 na kuifungia mabao 60. Kijana huyo wa umri wa miaka 24, anaondoka Mazembe akiiachia taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku naye akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika.
Zacharia Hans Poppe amejitolea kwa mapenzi yake kuijengea Simba Uwanja wa mazoezi |
Samatta akiwa na bahasha ya burungutu la fedha alilokabidhiwa na Waziri wa Nyumba Ardhi na Maendelea Wiliam Lukuvi (kushoto) pamoja na hati ya kiwanja (katikati) ni Waziri wa Habari na Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye
Ingawa bado klabu yake, TP Mazembe haijatangaza rasmi, lakini taarifa zinasema mwishoni mwa mwaka jana, Rais wa klabu hiyo ya Lubumbashi, Moise Katumbi alifikia makubaliano na klabu hiyo ya Ubelgiji juu ya biashara ya mchezaji huyo. Samatta aliyejiunga na TPM mwaka 2011 akitokea Simba SC aliyoichezea kwa nusu msimu, akitokea African Lyon, anaondoka Mazembe baada ya kuichezea mechi 103 na kuifungia mabao 60. Kijana huyo wa umri wa miaka 24, anaondoka Mazembe akiiachia taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, huku naye akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika.
chanzo : www.binzubeiry.co.tz
No comments:
Post a Comment