LILIPOFIKIA BEEF LA DIAMOND NA KIBA - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 23 August 2017

LILIPOFIKIA BEEF LA DIAMOND NA KIBA




Stori kubwa kwa sasa kwenye mitandao Tanzania ni inayodaiwa kuwa ni beef kati ya mastaa wa Bongofleva, Diamond Platnumz na Alikiba ambapo kumekuwa na majibizano huku Diamond Platnumz akitumia baadhi ya maneno yanayodaiwa kuwa ni vijembe.

Kwenye kipisi kingine cha ngoma aliyoachia Diamond kwenye Instagram hakumtaja mtu lakini Diss hiyo ilitafsiriwa kuwa ni imeenda kwa Alikiba na Ommy Dimpoz ikisema >>> “kufanya verse moja tu naona povu linawashuka, kina dada wavaa top na vibukta.. hawatoi ngoma kazi Twitter kunisuta"

Sasa baada ya hiyo Diss Ommy Dimpoz aliweka picha kwenye Instagram yake akiwa na Mama mzazi wa Diamond Platnumz na kuandika haya maneno hapa chini ambapo post hiyo imemfanya Mubenga kujitokeza na kumwambia kuwa hakupaswa kumuhusisha mpaka mama.

Mubenga aliandika >>>“Omary mdogo wangu maandiko yanasema waheshimu wazazi upate heri na Miaka mingi duniani na mzazi sio mpaka akuzae ata mzazi wa mwenzio pia ni mzazi wako why unamuingiza mama naseb kwenye mambo yenu? Uko ni kukosa adabu wew si unajifanyaga innocent kwa watu kumbe una pretend? Wew sindio uliyeimba nani kama mama imekuwaje leo una watusi wa kina mama

Au ndio stress za mziki? Watu wanataka video ya cheche na sio kutusi wazazi wa watu usituaribie muziki wetu kama game imekushinda please kaa pembeni pia naomba vyama vyenye dhamana ya muziki vichukue atua kali zidi ya matusi ya omary kwa mama wa diamond ili iwe fundisho kwa wengine ya kwangu ni hayo tu!  – Mubenga

No comments:

Post a Comment